The Big Boss
| The Big Boss | |
|---|---|
Sura ya filamu ya Hong Kong | |
| Imeongozwa na | Lo Wei, Wu Chia-hsiang |
| Imetayarishwa na | Raymond Chow |
| Imetungwa na | Lo Wei |
| Nyota | Bruce Lee, Maria Yi, James Tien, Han Ying-chieh |
| Muziki na | Wang Fu-ling, Peter Thomas |
| Sinematografi | Chen Ching-chu |
| Imehaririwa na | Sung Ming |
| Imesambazwa na | Golden Harvest |
| Imetolewa tar. | 23 Oktoba 1971 (Hong Kong) |
| Ina muda wa dk. | Dakika 100 |
| Nchi | Hong Kong |
| Lugha | [[Lugha ya Cantonese, Mandarin, Thai|Cantonese, Mandarin, Thai]] |
| Bajeti ya filamu | US$ 100,000 |
| Mapato yote ya filamu | US$ 50,000,000 |
| Ikafuatiwa na | Fist of Fury |
The Big Boss (kwa Kichina: 唐山大兄; huko Marekani inajulikana kama Fists of Fury) ni filamu ya mapigano ya mwaka 1971 kutoka Hong Kong iliyoongozwa na Lo Wei. Hii ni filamu ya kwanza kubwa kwa Bruce Lee kucheza kama mhusika mkuu tangu arudi katika tasnia ya filamu ya Hong Kong mwaka 1960. Filamu hii pia imewashirikisha waigizaji kama Maria Yi, James Tien, na Nora Miao.
Hapo awali, nafasi ya mhusika mkuu ilipangwa kuchezwa na James Tien, lakini baada ya mwongozaji kubadilishwa na kuwa Lo Wei, nafasi hiyo alipewa Bruce Lee. Bruce Lee alionyesha uwezo mkubwa wa kuigiza ambao ulimfunika James Tien (ambaye tayari alikuwa staa mkubwa wakati huo), na jambo hili lilimfanya Bruce Lee kuwa maarufu sana Kusini Mashariki mwa Asia na baadaye duniani kote.
Filamu hii ilipata mafanikio makubwa sana sokoni. Ikiwa na bajeti ndogo ya takriban dola 100,000, ilifanikiwa kuingiza karibu dola milioni 50 duniani kote. Hiyo ni mara 500 zaidi ya gharama iliyotumika kuitengeneza! The Big Boss ilishikilia rekodi ya kuwa filamu iliyoingiza pesa nyingi zaidi nchini Hong Kong hadi ilipokuja kupitwa na filamu nyingine ya Lee iitwayo Fist of Fury mnamo mwaka 1972.
Mkasa
[hariri | hariri chanzo]Cheng Chao-an, kijana mgeni kutoka vijijini nchini China, anahamia Pak Chong, nchini Thailand, kuishi na ndugu zake na kufanya kazi katika kiwanda cha barafu. Anakutana na binamu yake, Hsu Chien, ambaye anamvutia baada ya kusimama kidete dhidi ya wahuni waliokuwa wakimpiga mdogo wake. Ingawa Cheng anatamani kusaidia, anajizuia kwa sababu alimuahidi mama yake kuwa hataingia kwenye mapigano, na huvaa mkufu wa johari (jade) kama ukumbusho wa ahadi hiyo.
Cheng anaanza kazi kiwandani. Siku moja, kitalu cha barafu kinapasuka kwa bahati mbaya na mfuko wa unga mweupe—ambao ni dawa za kulevya—unaanguka. Binamu wawili wa Cheng wanauokota, na usiku huo wanaitwa na meneja ambaye anawaambia kuwa kiwanda hicho ni kichaka cha biashara ya magendo inayongozwa na Hsiao Mi (Big Boss). Ndugu hao wanapokataa kujiunga nao, wanauawa na miili yao kufichwa. Hsu Chien na binamu mwingine, Ah Pi, wanaenda nyumbani kwa Big Boss kutafuta ndugu zao, lakini nao wanauawa baada ya mapigano makali. Kukosekana kwao kunasababisha wafanyakazi kugoma na kuanza fujo dhidi ya uongozi wa kiwanda.
Cheng anaendelea kuvumilia, lakini wakati wa fujo hizo, mmoja wa wahuni anapasua mkufu wake wa johari. Kwa hasira, Cheng anaingia vitani na kuwapiga wahuni hao vibaya. Ili kutuliza hali, meneja anamteua Cheng kuwa msimamizi (mnyampara). Usiku wa sherehe ya uteuzi wake, Cheng anapewa pombe nyingi na kulala na mwanamke mmoja anayeuza mwili, Sun Wu Man. Jambo hili linamfanya aone haya mbele ya rafiki yake, Chow Mei, na anashindwa kutekeleza ahadi yake ya kufuatilia polisi kuhusu ndugu zake waliopotea.
Baadaye, Sun Wu Man anamwonya Cheng kuwa maisha yake yako hatarini na kumpa siri kuwa Hsiao Mi anajishughulisha na biashara ya dawa za kulevya. Baada ya Cheng kuondoka, mtoto wa Big Boss anamuua Sun. Cheng anavamia kiwandani na kugundua dawa za kulevya pamoja na vichwa vya ndugu zake na Sun vikiwa vimegandishwa kwenye barafu. Cheng anapigana na kuua kundi la wahuni pamoja na mtoto wa Big Boss, kisha anarudi nyumbani na kukuta ndugu zake wengine wote wameuawa na Chow Mei ametekwa.
Akiwa na uchungu mkubwa, Cheng anaapa kulipiza kisasi. Anavamia jumba la Big Boss na kupigana na kundi lake lote. Wakati mapigano yakiendelea, mtumwa mmoja wa Big Boss anamwachia huru Chow Mei, ambaye anakimbia kwenda kuita polisi wa Thailand. Baada ya mapambano makali ya ana kwa ana, Cheng anamuua Big Boss kwa kumchoma kisu. Baada ya kuona Chow Mei yuko salama akiwa na polisi, Cheng anajisalimisha mikononi mwa mamlaka.
Washiriki
[hariri | hariri chanzo]- Bruce Lee
- James Tien
- Nora Miao
- Lee Kwan
- Han Ying-chieh (The Big Boss)
- Tony Liu
- Kam San
- Kam San
- Li Hua Sze
- Malarin Boonak
- Chan Chue
- Chom
- Billy Chan Wui-ngai
- Lam Ching-ying
- Tu Chia-Cheng
- Peter Chan Lung
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The Big Boss at the Internet Movie Database
- The Big Boss at Rotten Tomatoes
- The Big Boss at the Hong Kong Movie DataBase
- (Kiingereza) The Big Boss katika Allmovie
- An in-depth article on the missing scenes featuring rare publicity shots and screenshots Ilihifadhiwa 23 Machi 2019 kwenye Wayback Machine.
| Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu The Big Boss kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |