Wasumbwa
Wasumbwa ni kabila la watu kutoka eneo la wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita, Kaskazini mwa nchi ya Tanzania. Pia kuna Wasumbwa katika mkoa wa Tabora: wanapatikana wilaya ya Kaliua, kata za Uyowa na Silambo, ambao
Mwaka 1987 idadi ya Wasumbwa ilikadiriwa kuwa 191,000[1].
Lugha yao ni Kisumbwa, jamii ya Kisukuma na Kinyamwezi. Wengi wao huzungumza lugha ya Kisumbwa lakini pia wanaishi pamoja na jamii ya Wasukuma, Wanyamwezi na Wahutu kwa sababu, wapo tarafa ya Ulyankulu ambayo ni makazi ya wakimbizi kutoka Burundi, hivyo kutokana na mwingiliano huo, Wasumbwa huweza kusikilizana na makabila hayo yote kwa sababu Wasumbwa wengi wameoa na kuolewa na makabila hayo yaliyowazunguuka. Pia Wasumbwa huweza kuzungumza na kusikilizana na Waha kutoka Kigoma kutokana na kuwa kabila hilo limepakana na wilaya hiyo na wafanyabiashara wengi waliopo Wilaya ya Kaliua wametokea Kigoma hasa eneo maarufu kama Uvinza na Mpanda.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Mtemi wa kabila la Wasumbwa katika eneo la Ushirombo, Kahama, Masumbwe mpaka Runzewe alikuwa Mtemi Lwassa ambaye alikutwa na utawala wa Wajerumani. Baadaye mtemi Lwassa alikimbilia Upuge, Mkoa wa Tabora kwa hofu ya kuuawa na Wajerumani ingawa baada ya Wajerumani kupata taarifa za mtemi Lwassa, utawala uliagiza kumrejesha Kahama ambayo ndiyo yalikuwa makao makuu yake kabla hajahamia Runzewe ambako ndiko alikofariki na kuzikwa katika eneo la Musasa, Runzewe Magharibi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wasumbwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |